Kama tayari una akaunti ya maombi ya kufungua Famasi, tafadhari bonyeza HAPA kuingia kwenye Mfumo (Login)

VIGEZO VYA KUZINGATIA KABLA KUFANYA MAOMBI YA KUFUNGUA FAMASI

(Made under Regulation 4&5 of the Pharmacy (Premises Registration) Regulations GN 269, 2020)



1. REJAREJA / COMMUNITY PHARMACY

  • i. Hakikisha kuwa ukubwa wa jengo si chini ya mita za eneo 30 (30m2)

  • ii. Hakikisha kuwa umbali kutoka famasi ya karibu ya rejareja si chini ya mita 150 (150m)

  • iii. Hakikisha kuwa eneo unalotaka kufungua lipo umbali wa mita 100 kutoka sehemu zisizofaa kwa huduma za famasi, mfano: - bar, kituo cha mafuta, mifereji ya maji taka iliyowazi, madampo, gereji na umbali wa mita 50 kutoka maabara

  • iv. Hakikisha kuwa umbali kutoka vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali unakuwa kamaifuatavyo;-

    • ✔ 500m kutoka Hospitali ya Taifa au Hospitali ya Kanda

      ✔ 400m kutoka Hospitali ya Mkoa

      ✔ 300m kutoka Hospitali ya Wilaya

      ✔ 200m kutoka Kituo cha afya au Zahanati

  • v. Ukijiridhisha jaza fomu ya maombi ya ukaguzi wa awali kwa umakini approval of location form – PCF.5a.

  • vi. Lipia TZS 100,000/= kwa njia ya Control number kwa ajili ya ukaguzi na upewe risiti ya Baraza.


2. JUMLA / WHOLESALE PHARMACY

  • i. Hakikisha kuwa ukubwa wa jengo si chini ya mita za mraba 60 (60m2)

  • ii. Fuata hatua (iii) – (vii) kama ilivyo hapo juu


3. ZINGATIA YAFUATAYO;-

  • i. Hutakiwi kufanya matengenezo yeyote kabla haujafanyiwa ukaguzi wa awali.

  • ii. Baraza lina mamlaka ya mwisho kuamua eneo linalofaa kwa biashara ya famasi, na ni jukumu la mwombaji kuhakikisha kuwa anazingatia vigezo vilivyoweka na Baraza.

  • iii. Hakikisha namba za simu unazojaza zinapatikana muda wote